📘 قراءة كتاب Namna ya swala ya mtume saw na Namna ya kutawadha أونلاين
Namshukuru Mwenyezi Mungu peke yake, rehema na amani
zimwendee mja wake na Mtume wake Mtume wetu Muhammad pamoja
na familia yake na Maswahaba zake.
Amma baad.
Haya ni maneno kwa ufupi yanayo bainisha namna ya swala ya
Mtume (s.a.w), nimekusudia kuileta kwa kila Muislamu mwanaume na
mwanamke ili ajitahidi kila atakae soma kitabu hiki amuige Mtume
(s.a.w) kwa ajili ya kufanyia kazi maneno yake Mtume (s.a.w): (Swalini
kama mlivyo niona nikiswali). Kapokea hadithi hii Imamu Bukhari.
Ni juu ya msomaji kufuata haya:
1: AUKAMILISHE UDHU.
Nako ni kutawadha kama alivyo amrisha Mwenyezi Mungu kwa
kauli yake tukufu: (Enyi mlio amini! Mnapo simama kwa ajili ya Sala
basi osheni nyuso zenu, na mikonoyenu mpaka vifundoni, na mpake
vichwa vyenu, na osheni miguu yenu mpaka vifundoni...). (Al-Maida: 6).
Na kauli ya Mtume (s.a.w): (Haikubaliwi swala bila ya
kujitwaharisha). Ameipokea hadithi hii Imamu Abuu Daud na Tirmidhiy,
na akaisahihisha Shekh Al-baniy (r.h).
Na udhu unakuwa kama ifuatavyo:
1: Anuwie kutawadha ndani ya moyo wake bila ya kutamka niya,
kwa sababu Mtume (s.a.w) hakutamka niya wakati wa kutawadha kwake
wala ndani ya swala yake wala katika ibada yake yoyote, kwa sababu
Mwenyezi Mungu anafahamu yaliyomo moyoni hakuna haja ya
kumwambia anayotaka kuyafanya.
2: Kisha aseme: (Bismi LLah).
3: Kisha aoshe vitanga vyake mara tatu.
4: Kisha aingize maji mdomoni na kusukutua na kupandisha
mengine puani na kuyatoa kwa mkono wake wa kushoto mara tatu.
5: Kisha aoshe uso wake kuanzia maoteo ya nywele mpaka chini ya
kidevu kwa urefu, na sikio hadi sikio kwa upana mara tatu.
6: Kisha aoshe mikono yake kuanzia mwanzo wa vidole mpaka
kwenye kongo mbili mara tatu, akianzia mkono wa kulia kisha wa
kushoto.
7:Kisha apake kichwani kwake mara moja, alowanishe vitanga
vyake vya mikono kisha apitishe kuanzia mwanzo wa kichwa chake
mpaka nyuma ya kichwa chake kisha arejeshe alipoanzia.
8: Kisha apake masikioni kwake mara moja, aingize vidole vyake
kwenye masikio yake na apitishe vidole gumba vyake nyuma ya masikio
yake.
9: Kisha aoshe miguu yake kuanzia mwanzo wa vidole mpaka juu
ya fundo mbili mara tatu, aanzie mguu wa kulia kisha amalizie wa
kushoto.
Amesema Mtume (s.w.a): (Hawi yeyote miongoni mwenu
anapotawadha na kukamilisha udhu kisha akasema: Ash-hadu anlaa
iLaha illa LLahu wahdahu laa sharika lahu, wa Ash-hadu anna
Muhammada abduhu wa rasuluhu, isipokuwa hufunguliwa kwa ajili yake
milango minane ya pepo ataingia katika mlango anaoutaka). Kaipoke
hadithi hii Imamu Muslim.
Kitabu hii kinaelezea sifa ya swala ya mtume s.a.w . na jinsi ya kutawadha, kitabu hiki nizawadi kwa waislam wote wanaotaka kumuiga mtume s.a.w katika swala na udhu.
سنة النشر : 2015م / 1436هـ .
حجم الكتاب عند التحميل : 447.3 كيلوبايت .
نوع الكتاب : pdf.
عداد القراءة:
اذا اعجبك الكتاب فضلاً اضغط على أعجبني و يمكنك تحميله من هنا:
شكرًا لمساهمتكم
شكراً لمساهمتكم معنا في الإرتقاء بمستوى المكتبة ، يمكنكم االتبليغ عن اخطاء او سوء اختيار للكتب وتصنيفها ومحتواها ، أو كتاب يُمنع نشره ، او محمي بحقوق طبع ونشر ، فضلاً قم بالتبليغ عن الكتاب المُخالف:
قبل تحميل الكتاب ..
يجب ان يتوفر لديكم برنامج تشغيل وقراءة ملفات pdf
يمكن تحميلة من هنا 'http://get.adobe.com/reader/'